Serikali
ya awamu ya tano kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imesema itafanya zoezi la
ukaguzi nchini nzima katika sehemu za kazi ikiwemo kampuni ya ACACIA
ili iweze kuwabaini waajiri ambao hawazingatii vigezo na masharti
wanayopaswa kuwafanyia wafanyakazi wao.
Kauli
hiyo imetolewa leo Mei 07, 2018 na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde Bungeni Jijini
Dodoma kwenye kikao cha 23 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la Mbunge wa viti maalum Jocye B.
Sokombi aliyetaka kusikia kauli ya serikali juu ya tatizo la wafanyakazi
wa mgodi wa Nyamongo kutolipwa mshahara wala posho pindi wafanyapo kazi
zao.
"Mgodi
wa dhahabu wa Nyamongo unamilikiwa na kampuni ya ACACIA na kwenye mgodi
huo kuna makundi mawili ya wafanyakazi ambapo moja ni wale walioajiriwa
na ACACIA na pili wafanyakazi waliajiriwa na makampuni yanayopewa kazi
na ACACIA 'sub contractors'. Hivyo kwa wafanyakazi walioajiriwa na
ACACIA wao hawalipwi posho bali hulipwa mshahara kwa mwezi", amesema
Mavunde.
Pamoja
na hayo, Mavunde ameendelea kwa kusema "makampuni mengine huwa
wanalipwa mishahara kutokana na aina ya mikataba ya ajira na asili ya
kazi anayoifanya mfanyakazi kwa kuzingatia sheria. Ofisi yangu kupitia
idara ya kazi itaendelea kufanya kaguzi za kazi katika sehemu za kazi
mbalimbali nchini ikiwepo kampuni ya ACACIA kwa lengo la kuwatambua
waajiri ambao hawazin gatii matakwa ya sheria za kazi yanayotakiwa".
Kwa
upande mwingine, Naibu Waziri Antony Mavunde amesema idara ya kazi
imekuwa na taratibu za kufanya ukaguzi katika makampuni yote kwa lengo
la kujua changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwa wafanyakazi.
Post A Comment: