Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kuwa ajali za barabarani husababishwa na vitu vikuu vitatu ambavyo ni vya kibinadamu kwa 76%, vyanzo kiufundi kwa 16% na vya Kimazingira kwa 8%.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, Bungeni Mjini Dodoma ambapo amesema kuwa asilimia za Kibinadamu vyanzo vingi vinakuwa ni uzembe.
“Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa na Jeshi la Polisi, ajali za barabarani husababishwa na vitu vikuu vitatu ambavyo ni vyanzo vya kibinadamu husababisha ajali kwa 76%, vyanzo vya kiufundi vinasabisha ajali kwa 16% ni vyanzo vya Kimazingira vinasababisha kwa 8% vyanzo vya kibinadamu ndio unakuta kuna uzembe kunakuwa vyanzo vingi, baadhi ya vijana wetu waendesha pikipiki bado wana uelewa mdogo kuhusu sheria za usalama barabarani na wengine pikipiki zina mapungufu mengi ambayo huwafanya kutojiamini wanapoendesha,” amesema Mwigulu.
Ameongeza “Kutokana na sababu hizi na nyinginezo waendesha bodaboda hujihisi wanamakosa wakati wowote wawapo barabarani na hivyo huwa na hofu ya kukamatwa na askari Polisi, ni wajibu wa polisi kuhakikisha sheria zinafuata na si kuvunjwa, waendesha pikipiki wanapaswa kutambua hilo na wao kutimiza wajibu wao wakufauta sheria hali ya kutambua wanamakosa ndio huwa fanya kukimbia askari na hata kama askari hana lengo la kuwakamata.”
Hata hivyo amesema kuwa Ili kuepukana na ajali za kizembe serikali kupitia Jeshi la Polisi itaendelea kutoa elimu kwa waendesha pikipiki ili kuwajengea uwezo wa usalama barabarani.
Post A Comment: