Serikali imesema kwamba barabara kuharibika mara kwa mara ni jambo la kawaida na hali hiyo inachangiwa na sababu mbalimbali ambazo hupelekea miundumbinu hiyo kuaribika.
Hayo yamesemwa leo Mei 04 na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Elias Kwandikwa katika kipindi cha maswali na majibu bungeni na kuongeza kuwa barabara hizo huwa na muda maalumu wa kuishi na ndiyo maana serikali hutenga fedha kwa ajili ya marekebisho.
“Ni kweli kuna baadhi ya maeneo baada ya barabara kutengenezwa zinaharibika, ni hali ya kawaida na ndio maana baada ya ujenzi katika kipindi cha maisha ya barabara tunatenga fedha kwa ajili ya kufanya marekebisho” amesema Kwandikwa.
Naibu Waziri amesema kuwa serikali huwa inafanya matengezo makubwa ya barabara kila baada ya miaka 20 tangu kukamilia kwa ujenzi husika kwasababu muda wa maisha ya barabara hiyo unakua umekwisha.
Naibu Waziri Kwandikwa, alikua akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Mariam Msabaha aliyetaka kujua serikali inachukua hatau gani kwa barabara ambazo zinaharibika muda mfupi baada ya ujenzi ya kukamilika.
Post A Comment: