Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema kuwa itayatengeneza na kuyauza magari yaliyorundikwa katika vituo vya Polisi ili kupunguza msongamano wa magari mabovu vituo humo.
Hayo yamebainishwa na Wizara hiyo, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa(CCM), Ritta Kabati aliyehoji, Katika mkoa weti wa Iringa Kuna magari ambayo yanaharibika tu kidogo yanawekwa katika vituo, unakuta sasa kuna mrundikano mkubwa wa magari mabovu sasa ni kwanini sasa serikali either au iyauze haraka sana ili yaweze kusaidia upungufu uliopo katika Mkoa wa Iringa?
“Niseme tu sisi kama serikali tunapokea ushauri huo tutayatengeneza yale yanayo yanatengenezeka na tutafanya utaratibu wa kuyauza yasiyoweza kutengenezeka,” amesema Mwigulu.
“Kwa upande wa pikipiki nilishatoa mapendekezo vijana hawa wa bodaboda wanaokamatwa kwa makosa madogo madogo wafanye utaratibu wa kuandikisha na kurudishiwa pikipiki zao na waweze kulipia kama kuna faini walikuwa wanatakiwa kulipa kuliko kuzirundika pikipiki hizo na kuendelea kuharibika.”
Post A Comment: