Mbunge
wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali amesema uamuzi wa Chuo Kikuu Dar es
Salaam (UDSM) kumsimamisha masomo mwanafunzi wake wa mwaka wa tatu,
Abdul Nondo unakitia aibu chuo hicho na ni kinyume na haki za binadamu.
Akizungumza
jana Jumatatu Aprili 30, 2018 wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia mwaka 2018/19, Bobali alisema sheria
iliyotumika kumsimamisha masomo inatakiwa kufutwa.
“Hivi
ni wanafunzi wangapi ambao wameshtakiwa na kesi zao zipo mahakamani
lakini wanaendelea na masomo. Hili suala la Nondo linakitia aibu chuo
pengine watueleze tu kwamba jambo hili ni la kisiasa,” alisema Bobali.
Wakati
Bobali akitoa maelezo hayo, mbunge wa Magogoni (CUF), Dk Ally Yusuf
Suleiman aliomba taarifa kwa Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge na
kubainisha kuwa hata wabunge wapo walioshtakiwa, wengine kufungwa lakini
mpaka sasa bado wanaendelea na ubunge wao.
“Napenda
kumpa taarifa mzungumzaji (Bobali) kuwa hata wabunge wapo walioshtakiwa
lakini mpaka kufungwa lakini bado ni wabunge hadi sasa,”alisema
Suleiman.
Nondo
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP)
amesimamishwa masomo kuanzia Machi 26, 2018 kwa barua iliyoandikwa na
Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye, aliyeeleza kuwa
amesimamishwa kwa mujibu wa taratibu za chuo hicho.
Nondo
alijikuta kwenye misukosuko na vyombo vya dola tangu alipotoweka katika
kile kilichoelezwa kuwa ni katika mazingira ya kutatanisha Machi 6 na
kuonekana Machi 7 wilayani Mufindi, Iringa.
Post A Comment: