Wakati kikosi cha Yanga kikitarajia kuanza safari yake kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger, kumekuwa na sintofahamu juu ya safari hiyo.

Licha ya sintofahamu iliyojitokeza, blog hii imefanya jitahada za hali na mali kutaka kujua namna Yanga walivyojiandaa kuanza safari hiyo lakini viongozi wamekuwa hawapokei simu.

Yanga itakuwa na kibarua dhidi ya wapinzani hao wa Algeria, USM Alger katika mchezo wa mkondo wa kwanza utakaopigwa Mei 6 2018 nchini humo.

Haijajulikana sababu za viongozi hao kutopokea simu kwa takribani lakini taarifa za chini ya kapeti zinaeleza kuwa baadhi ya wachezaji wameweka mgomo kutokana na kutolipwa stahiki zao ikiwemo mishahara.

Hata hivyo uongozi licha ya kushindwa kupokea simu, leo umetangaza kuitisha kikao na Waandishi wa Habari kitakachofanyika majira ya saa 6 mchana kwenye makao makuu ya klabu.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: