Tukio gani la Ronaldinho unalikumbuka? Basi achana na hilo, mchezaji huyo wa zamani wa Brazil na vilabu vikubwa Ulaya, amepanga kuushangaza ulimwengu mwaka huu – Mchezaji huyo anatarajia kufunga ndoa siku moja na wapenzi wake wawili kwa pamoja.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Brazil, vimeripoti kuwa Gaucho amepanga kufunga ndoa na wapenzi wake hao Priscilla Coelho na Beatriz Souza mwezi August mwaka huu.
Ronaldinho akiwa na wapenzi wake Priscilla Coelho na Beatriz Souza
Vyombo hivyo vimeongeza kuwa mchezaji huyo anaishi nyumba moja na warembo hao katika jumba lake la kifahari lililopo mjini Rio de Janeiro, ambalo linathamani ya paundi milioni tano ambapo ni zaidi ya shilingi bilioni 15 za Kitanzania.
Inadaiwa kuwa Ronaldinho ameanza kuishi pamoja na wapenzi wake hao tangu Disemba 2016. Hata hivyo dada wa mchezaji huyo amesema kuwa hajaridhishwa na harusi hiyo
Post A Comment: