Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo, leo amewaongoza maelfu ya wananchi mkoani hapa kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambayo Kimkoa shamra zake zilifanyika katika Uwanja wa Sheik Amri Abeid.
Wafanyakazi wa serikali na makampuni mbalimbali binafsi walijumuika pamoja kusherehekea siku hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo (wa tatu kushoto) akiwa amefuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini Mh: Fabian Daqarro pamoja Katibu Tawala wa Mkoa Richard Twitega na viongozi wa wafanyakazi serikali, mashirika ya umma na taasisi binafsi Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Post A Comment: