Wanafunzi
wa Chuo cha Kilimo cha Kilimo cha Sokoine (SUA) wametoa ya moyoni mbele
ya Rais John Magufuli kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo chuoni
hapo ikiwamo uhaba wa mabweni ya wanafunzi na fedha za mikopo.
Wametoa
ya moyoni baada ya kiongozi huyo mkuu wa nchi kutoa nafasi kwa
wanafunzi na watumishi wa chuo hicho kueleza mambo mbalimbali
wanayokabiliana nayo baada ya kufanya ziara katika chuo hicho kilichopo
mjini Morogoro.
Kabla
ya Rais kutoa nafasi hiyo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Profesa Joyce Ndalichako alieleza mafanikio na juhudi zinazoendelea
kufanywa na wizara yake ikiwa ni pamoja na kufanikisha utoaji wa mikopo.
Hata
hivyo, Emmanuel Gwalaje, mwanafunzi wa mwaka wa kwanza kozi ya wanyama
amesema wapo wanafunzi wa mwaka wa kwanza chuoni hapo hawajalipwa fedha
katika muhula wa kwanza na wanaishi maisha magumu hadi sasa.
Mhadhiri
wa chuo hicho, God Swai amesema wanafunzi wanaporwa mitaani na kukabwa
kutokana na uhaba wa majengo ya bweni, huku akiomba kujengwa kwa ofisi
za wahadhiri chuoni hapo.
Mbali
na maombi ya wanafunzi, pia kulikuwa na maombi ya watumishi, huku Amina
Juma akiomba Rais Magufuli kuwafikiria watumishi wa darasa la saba
waliofukuzwa kazi.
Amesema
yeye ni mtumishi chuoni hapo tangu mwaka 1994, aliyeathirika na
kuondolewa kwa watumishi wa darasa la saba, akiomba wafikiliwe upya
kutokana na hali ngumu ya maisha mtaani.
Post A Comment: