Rais John Magufuli amefichua siri ya kukataa kuweka jiwe la msingi katika ukumbi wa jengo lililopo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa mkoani Iringa akisema limejengwa kifisadi kwa Sh 8bilioni.

Rais ameeleza hayo jana, Mei 2, 2018 wakati akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani humo.

"Muda mwingine tuambizane ukweli Chuo cha Mkwawa kimeniangusha, ndio maana nilikataa kuja kuweka jiwe la msingi katika lile jengo. Siwezi kuweka jiwe la msingi katika jengo la kifisadi.

"Nikitoka hapa nitakwenda kulikagua. Nilitegemea chuo hiki kitasimamia value of money (thamani ya fedha), kwa sababu kuna wasomi lakini tofauti."

Rais Magufuli alitumia nafasi hiyo kuviagiza vyombo vya dola kuhakikisha wanawachukulia hatua wale wote waliohusika katika mchakato huo hata kama wamestaafu, watafutwe waliko.

"Mmeshindwa kusimamia ujenzi wa lile jengo halafu leo mnaniomba mabweni? Nitaanzaje kuwakubalia wakati huku mmeshindwa, siwezi. Vyombo vya dola  na wizara vifuatilie mkishindwa nitafuatilia.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: