Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amesema jalada la uchunguzi wa watu wanaosambaza vitabu mitandaoni limefunguliwa.
Akizungumza jana Ijumaa Mei 4, 2018 katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Kamanda Sirro amesema wamepokea maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.
"Tumepokea maelekezo na tayari tumefungua jalada na tutakapowapata tutawapeleka mahakamani," alisema IGP Sirro.
Kuhusu watu wanaovunja sheria ya mitandao, IGP Sirro amesema wanaendelea kufuatilia na kila atakayekuwa anabainika wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Post A Comment: