Muonekano wa sasa wa  kituo cha Afya Usa - River  Kilichopo  Halmashauri ya Wilaya ya Meru ni matumaini  ya upatikanaji wa huduma bora  za afya kwa wananchi ,muonekano huu unatokana na ujenzi wa miundombunu mbalimbali ulioanza mwezi Februari 2018. 


==>> Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>

Aidha ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwenye  kituo hicho cha Afya Usa -River  ni baada ya Serikali kutoa fedha kiasi cha Sh. milioni 500 kwa ajili ya kuboresha kituo hicho kwa kujenga majengo  mapya ambayo ni jengo la maabara,nyumba ya mtumishi, jengo la upasuaji, wodi ya mama na mtoto, chumba cha kuifadhia maiti, kichomea taka  pamoja na kufanya ukarabati wa majengo yaliyokuwepo kwa lengo la kuwapa wananchi huduma bora za afya na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi. 

picha zifuatazo zinaonesha baadhi ya  ujenzi wa majengo mapya na ukarabati unaoendelea ukiwa kwenye hatua za mwisho 



Jengo la wodi ya Mama na Mtoto ,pindi litakapo kamilika kinamama zaidi ya 40 watakaojifungua kwenye kituo hicho wataweza kupata malazi kwa wakati mmoja  .
mwonekano wa mbele wa Jengo la wodi ya Mama na Mtoto ,
Sehemu ya kufulia kwenye Jengo la wodi ya Mama na Mtoto  ikiwa na uhakika wa upatikanaji wa maji wakati wote kutokana na uwepo wa matanki ya kuifadhia maji .
Mwonekano wa ndani wa Jengo la wodi ya Mama na Mtoto  
Mwonekano wa ndani wa Jengo la wodi ya Mama na Mtoto  sehemu ya choo..
 Jengo la upasuaji pindi litakapoanza kutumika kwa kiasi kikubwa litapunguza vifo vitokanavyo na uzazi pamoja na msongamano wa wagonjwa kwenye Hospitali ya Wilaya.

Nyumba ya mtumishi itaboresha mazingira ya mtumishi kufanya kazi kwenye mazingira rafiki hivyo huduma za dharura kupatikana kwa urahisi.
Jengo la Maabara litaongeza  huduma za uchunguzi wa kimaabara  .
Muonekano wa ndani wa Jengo la Maabara  .
  Jengo la kuifadhia maiti .                                                                 

Jengo hili kabla ya ukarabati lilikuwa na pande mbili likitumika kama wodi ya wanawake na wanaume  .                                                                                                                                                                                                                                           
Marekebisho ya Jengo la kuwahudumia wagonjwa wa wa nje  (OPD)
 Marekebisho ya jengo la duka la dawa ambalo awali lilitumika kama kama jengo Maabara.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: