Mwanamuziki wa Bongo fleva Nandy amefunguka na kudai alikuwa tayari kuacha muziki baada ya ile video yake chafu kuvuja Kwenye mitandao ya kijamii.

Wiki chache zilizopita Nandy aliwaacha watu midomo wazi baada ya video yake iliyomuonyesha akiwa kitandani na aliyekuwa mpenzi wake Billnas kuvujishwa Kwenye mitandao ya kijamii.

Nandy amekiri kutaka kuacha muziki Kwenye mahojiano na Kipindi cha leo Tena cha Clouds Fm ambapo amesema;

"Nilihisi kukata tamaa na  kuachana na muziki kabisa  maana sikuona maana ya maisha. Lakini nilipofika BASATA walinipa ushauri na kunihoji kama kweli nilivujisha picha zile kwa ajili ya Kiki, ... binafsi sikuwa na picha mbaya nyuma katika maisha yangu

"  Hali yangu ilikuwa mbaya sana nilipoona ile video sikuamini kabisa macho yangu. Nilizidiwa na Pumu nikakimbizwa hospitali kifupi nilipata Brain Attack niliwaza kuhusu familia yangu nItamtazamaje mama na baba yangu?”.

Nandy jana aliachia wimbo wake mpya ulioandikwa na msanii mwenzake Aslay unaoitwa Ninogeshe.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: