Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka THT Nandy amekiri kuwa pamoja na mambo mengine yote na maneno yakiwekwa pembeni staa wa Bongo fleva Ali Kiba amemu-insipire sana kwa kinywaji chake.

Nandy amekiri kuwa hatua aliyofikia Ali Kiba ya kuingiza kinywaji chake mtaani ambayo ni Energy drink ni hatua kubwa sana ambayo imempa changamoto hata yeye ya kufanya makubwa zaidi.

Kwenye mahojiano aliyofanya na The Playlist ya Times, Nandy amekiri kuwa kupitia Kiba ni vizuri wasanii wengi wakajifunza kuwa ni vizuri kuwekeza nje ya muziki.

"Ameni-inspire kwa kinywaji kwa sababu ukiangalia the package ya kinywaji chake jinsi ilivyo ni project fulani ambayo ipo serious”.

Lakini pia Nandy ameongelea uwekezaji wa wasanii wengine kama Diamond Platnumz ambaye ni mmoja kati ya msanii Lakini pia mfanyabiashara.

"Tunaambiwa nje ya kuimba tunatakiwa tuwekeze nje ya muziki wetu na ndicho hiki kaka zetu wanafanya ukimuangalia kama Diamond, Alikiba ni vitu ambavyo wanatuhamasisha”.

Kwa hivi sasa Nandy anafanya vizuri sana ngoma yake ya Ninogeshe inayoshika namba moja kwenye mtandao wa Youtube.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: