Naibu Spika Dk. Tulia Ackson mwansasu amekabidhi misiti miwili ya kisasa kwa waumini wa dini ya kiislamu katika miji ya kiwira na tukuyu wilaya ni rungwe ambayo amewajengea baada ya miskiti yao ya awali kuwekewa alama ya X na hivyo kutakiwa kuvunjwa ili kupisha upanuzi wa barabara kuu ya Tanzania – Malawi.
Dk. Tulia Ackson Mwansasu ametimiza ahadi yake ya kushirikiana na waumini wa dini ya kiislamu katika miji ya Kiwira na Tukuyu wilayani Rungwe kwa kutafuta wafadhili ambao wamejenga misikiti mipya ndani ya muda mfupi kwa ajali ya waumini hao kufanyia ibaada baada ya misikiti yao ya awali kutakiwa kuvunjwa ili kupisha upanuzi wa barabara kuu iendayo malawi.
Akipokea misikiti hiyo kwa niaba ya waumini wa dini ya kiislamu,mwakilishi wa Sheikh mkuu wa mkoa wa Mbeya, Sheikh Hussein Katanga akiwataka waislamu kutumia nyumba hizo za ibada kumuabudu Mungu na kudumisha amani ya nchi.
Misikiti hiyo imejengwa kwa ufadhili wa Taasisi ya Human life Foundation ambapo mwakilishi wake, Sheikh Khalid Khalid amesema misikiti hiyo itumike kuleta neema kwa waislamu na wasio waslamu.
Post A Comment: