Hatimaye mwanasayansi wa Australia mwenye umri wa miaka 104, David Goodall ametimiza azma yake ya kujiua katika kliniki moja nchini Uswisi leo.
Awali, mtaalam huyo wa masuala ya mimea na ikolojia alikuwa analalama kuwa amechoka kuishi, hivyo hana sababu ya kuendea kuishi. “Maisha yangu yalikuwa kwenye kwenye kazi, sasa siwezi kwenye nje kufanya kazi,” CNN ilimnukuu mzee huyo.
Mzee David Goodall akisherekea siku yake ya kuzaliwa mapema mwezi April
Kabla ya kusafiri kutoka Australia kwenda Uswisi ili asaidiwe kufa, alifanya harakati za kuhalalisha mtu kusaidiwa kufa lakini mara iliposhindikana, aliamua kwenda kwenye nchi ambayo sheria zinatoa haki hiyo na kliniki moja huko Basel ndiyo iliyosikia kilio cha kikongwe huyo.
Siku mbili kabla ya kufariki, mwanasayansi huyo aliiambia CNN kuwa imefika mwaka wa kumi sasa tangu alipoacha kusikia furaha na kinachomuuma zaidi ni kwamba mzee huyo hawezi kutembea huku akisumbuliwa na macho
Post A Comment: