Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika CAF limemteuwa mwamuzi wa Ghana, Daniel Nii Ayi Laryea kusimamia mchezo wa klabu ya USM Alger ya nchini Algeria dhidi ya Yanga SC michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika utakao pigwa siku ya Jumapili.
Nii Ayi Laryea atasimamia mchezo huo wa kundi D, kwa kushirikiana na Abel Baba pamoja na David Laryea kutoka Nigeria.
Siku ya Jumatano, Daniel  alishuka dimbani kuchezesha mchezo wa ligi kuu nchini Ghana kati ya Berekum Chelsea dcidi ya WAFA kwenye dumb la Tema Sports.
Tayari Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga imeshakwea pipa capo jana siku ya Alhamisi kuifuata time hiyo ya Algeria kenye mchezo wake wa kwanza hate ya makundi unatao tarajiwa kuchezwa uwanja wa Stade 5 Juillet 1962  Mei 6 siku ya Jumapili.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: