Na James Timber, Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amekipongeza Kikosi cha Timu ya wanawake cha Tanzania Street Children (TSC), kwa kuja na Kombe la Mshindi wa pili nchini.

Mongella alisema kuwa ni jambo  jema hawakudanganya kwani walitoa ahadi hiyo ya ushindi na  kweli wamekuja  kombe kutoka nchini Urusi ambapo amewataka wachezaji hao kulinda heshima hiyo waliyonayo.

Rais wa TSC Hiran Mansoor, alisema kuwa  wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano mbalimbali huku kupitia vipaji  hivyo baadhi yao wamepata fursa ya kuendelezwa kielimu.
“Naipongeza kwa ushindi huo kwani  TSC imekuwa kitovu cha kuibua na kuendeleza vipaji ambapo baadhi ya wachezaji  wanachezea timu mbalimbali ikiwemo ya Simba," alisema Mansoor.

 Timu hiyo ya soka ya wasichana wanaoishi katika mazingira magumu TSC Sport Academy (Tanzania Street Children) ilipokelewa kwa kishindo katika uwanja wa ndege wa jijini hapa baada ya kushika nafasi ya pili ya  michuano ya kombe la dunia 2018 ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu  ambapo yalufanyika nchini Urusi.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: