Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe kuwa ataendelea kupaza sauti kupigania haki za wafanyakazi.

Zitto ametumia mitandao yake ya kijamii kueleza hayo, ikiwa leo ni siku ya wafanyakazi amewatakiwa Kila la kheri Wafanyakazi wote nchini huku akiwataka kutimiza wajibu wa kuleta mabadiliko.
Mei Mosi 2018: Kila la kheri Wafanyakazi wote nchini. Tutimize wajibu wa kuleta mabadiliko
Zitto Kabwe
Licha ya kwamba Wafanyakazi rasmi ni 9% tu ya nguvu kazi ya nchi yetu, ( kwa kigezo cha Kodi ya Mapato ), Wafanyakazi kupitia PAYE wanachangia 75% ya Kodi ya Mapato inayokusanywa na Serikali. Waajiri kupitia kodi za makampuni ( taxes on incomes/interests, profits and capital gains ) huchangia 25% tu.
Wafanyakazi wanaumizwa na mzigo wa kodi kwa sababu hawana fursa za kukwepa kodi kisheria maana kodi zao hukatwa moja kwa moja kutoka kwenye mishahara yao tofauti na wenye mitaji ambao huweza kukwepa kodi kwa mujibu wa sheria.
Tutaendelea kupaza sauti kupigania haki za Wafanyakazi, kuhakikisha Uchumi unazalisha ajira rasmi nyingi zaidi na mazingira ya Kazi kuboreka.
Tunatuma salaam za mshikamano kwa tabaka la Wafanyakazi nchini Katika siku hii muhimu kwao. Wafanyakazi kwenye sekta rasmi wanaofikia 2.1 milioni ni jeshi kubwa la kuleta mabadiliko nchini kwetu. Tutimize wajibu huo.
Mapambano yanaendelea. Mshikamano daima.
Kiongozi wa Chama
ACT Wazalendo
1/5/2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: