Arsenal
wameimarisha ofa yao kwa kiungo wa kati Jack Wilshere. Mkataba wa
mchezaji huyo wa miaka 26 unafikia kikomo mwisho wa msimu na amekuwa
akitafutwa na Wolves na Everton. (Mirror)
Mchezaji
anayesakwa sana na Liverpool Max Meyer hatachezea tena Schalke baada
yake kufukuzwa kutoka mazoezini na kutoka kwenye kikosi cha kwanza.
Meyer, mshambuliaji mwenye miaka 22, aliadhibiwa baada yake kumkosoa
mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ya Bundesliga Christian Heidel. (Sky
Sports)
Rais
wa Real Madrid Florentino Perez amesema Gareth Bale, 28, anataka
kusalia Bernabeu licha ya tetesi kwamba huenda mshambuliaji huyo wa
Wales akahama. (Sun)
Pep
Guardiola amesema uamuzi ufaao utafanywa kuhusu kipa wa Manchester City
Joe Hart iwapo West Ham wataamua kutobadilisha mkataba wake wa sasa wa
mkopo kuwa uhamisho wa kudumu. (Mirror)
Marouane
Fellaini, 30, anataka Manchester United wampe mkataba wa muda mrefu
zaidi kushinda mwaka mmoja ambao wamemuahidi kwa sasa Old Trafford.
(ESPN)
Kiungo
wa kati wa Arsenal Santi Cazorla anatumai kwamba ataweza kurejea
kucheza kabla ya mwisho wa msimu. Mhispania huyo mwenye miaka 33
hajachezea Gunners tangu mwaka 2016 kutokana na jeraha la mguuni ambalo
limekosa kupona. (AS)
Meneja
wa Shakhtar Donetsk Paulo Fonseca amekataa ofas kutoka kwa Everton
baada ya kuanza kuangazia kumrithi Arsene Wenger Arsenal, kwa mujibu wa
mwanahabari Guillem Balague. (Express)
Thierry
Henry na Tony Adams ni miongoni mwa watu mashuhuri 100 wa Arsenal ambao
wamealikwa kwa mechi ya mwisho ya Wenger nyumbani, ambapo
watasherehekea miaka 22 ya Mfaransa huyo katika klabu hiyo. (Mail)
Mshambuliaji
wa West Ham Andy Carroll, 29, alifukuzwa kutoka mazoezini Jumatatu na
meneja wa klabu hiyo David Moyes baada ya wawili hao kukorofishana.
Klabu hiyo inatarajiwa kuanza uchunguzi kuhusu kisa hicho. (Telegraph)
Imeandaliwa na BBC
Post A Comment: