Mbunge wa Iringa mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa fedha kusaidia jimbo lake katika uboreshaji wa miundo mbinu ikiwemo Barabara.
Tokeo la picha la MCHUNGAJI MSIGWA NA RAIS MAGUFULI
Mchungaji Peter Msigwa na Rais Magufuli (kulia kwenye picha)
Mchungaji Msigwa amesema hayo jana May 02, 2018 usiku kwenye hafla ndogo iliyoandaliwa na Rais Magufuli katika Ikulu ndogo mkoani Iringa ambapo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kisiasa na dini.
Mhe. Rais umekuwa ukisistiza katika hotuba zako kuwa wewe hujali mambo ya vyama, na hili umedhirisha kuwa hujali mambo ya vyama. Umesaidia sana hela za kutoka kwako zimekuja nyingi kama Mhe. Mahiga kuna barabara nzuri katika kipindi chako umekuwa Rais, umejenga barabara ya lami kutoka Mlandege hadi kwa mKuu wa Wilaya karibu bilioni 3.5 zimetumika. Kuna stendi nzuri ya Ipogolo karibu shilingi bilioni 3 zimetumika, kuna maji kwa hiyo kuna vitu vingi vimetumika kwa kweli Mhe. Rais hupendelei. Hela zinakuja hata kwa sisi ambao ni wa CHADEMA unaleta hela, kwahiyo tunakupongeza sana.“amesema Mchungaji Msigwa mbele ya Rais Magufuli.
Rais Magufuli amekuwa mkoani Iringa kwa ziara ya siku tano ambapo leo anatarajiwa kumaliza ziara yake na tayari ameshafungua miradi mikubwa ukiwemo mradi wa barabara ya Iringa-Migoli-Fufu yenye kilometa 189 na uliogharimu shilingi Bilioni 207.457.
Soma taarifa zaidi:

Share To:

msumbanews

Post A Comment: