Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP).
Taarifa hiyo imetolewa leo asubuhi Mei 11, 2018 bungeni mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge na kubainisha kuwa mbunge huyo kijana amechaguliwa jana kwa kishindo.
==>> Unaweza Kuidownload << kwa Kubofya Hapa>>
“Umelipa Bunge letu sifa na Tanzania kwa ujumla. Nafasi hii ni ya kuitangaza nchi yetu na Bunge hili tunamtakia kazi njema,” amesema Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi (CCM).
“Nampongeza sana kijana huyu, lakini pia Serikali kwani huwezi kupata nafasi hii kubwa kama huungwi mkono na Serikali. Nimpongeze sana Rais John Magufuli.”
Post A Comment: