Kikosi cha Mbao FC kitakuwa mgeni wa Yanga katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya Ligi Kuu Bara utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo Jumanne.

Mbao ambao wamekuwa wakipambana kuepuka kushuka daraja wameahidi kupigania alama tatu muhimu dhidi ya wapinzani wao Yanga ambao hawajapata ushindi katika michezo 9 iliyopita.

Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Fulgence Novatus, amesema kuwa wamejipanga vilivyo kukipiga na Yanga huku akieleza wanahitaji alama tatu muhimu.

Mbao FC ipo nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi hivi sasa ikiwa imejikusanyia alama 30 huku Yanga wakishika ya pili na alama zao 48.

Mbao imekuwa ikiisumbua Yanga mara nyingi zinapokutana tangu ipande Ligi Kuu na itaingia kucheza na Yanga ikiwa na kumbukumbu ya ushindi kwenye mchezo uliopita wa mabao 2-0 uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: