Jeshi la Polisi mkoani Tabora linamtafuta mtu mmoja aliyetajwa kwa jina la Omari Matonya kwa tuhuma za kumchinja mama na mtoto wake kisha naye kutoroka kusikojulikana.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Kamishina Msaidizi Mwandamizi Wilbrod Mutafungwa na kusema tukio hilo linadaiwa limetokana na wivu wa kimapenzi
Katika hatua nyingine Jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Kiwere Wilayani Sikonge Mkoani humo baada ya kumkamata na silaha nane za moto aina magobore ambazo zinasadikiwa kutumika katika kufanya ujangili katika hifadhi ya wanyama wilayani Sikonge.
Kamanda Mtafungwa amemtaja mtu huyo kwa majina ya Ibrahimu Yohana mwenye umri wa miaka 40 ambapo silaha hizo alizokamatwa nazo haikujulikana zinatumika kwa kazi gani.
Kwa upande mwingine, Kamanda Mtafungwa amesema uchunguzi wa kesi hiyo ukikamilika mtuhumiwa huyo atapandishwa Mahakamani.
Post A Comment: