Msemaji wa klabu ya Ruvu Shooting , Masau Bwire, jana alihudhuria kimyakimya mchezo wa ligi kati ya Yanga na Mbao FC uliofanyika Uwanja wa Taifa.
Baada ya kuhudhuria mechi hiyo, Bwire amefunguka kwa kueleza kuwa kwa namna alivyowaona Yanga wasitarajie kupata ushindi mbele yao.
Bwire ametamba akisema jinsi mpira wanaoucheza Yanga kama wakijitahidi zaidi watafungwa bao tatu badala ya nne.
"Kwa mpira huu waliocheza Yanga leo, hakika wasitarajie ushindi. Kwa namna nilivyowaona walivyocheza, siku wakicheza na sisi kama wakikaza sana basi watakula tatu badala ya bao nne" alisema Masau Bwire.
Ratiba ya ligi inaonesha Yanga itakuwa mwenyeji kwenye Uwanja wa Taifa kucheza na Ruvu Ijumaa ya wiki hii.
Post A Comment: