Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye amekaribisha uraini Mbunge wa Mbeya Mjini,Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ baada ya kutoka gereza la Ruanda alipokuwa akitumikia kifungo chake .
Nape amesema kuwa anakumbuka Mbunge huyo ambaye pia ni msanii aliwahi kuimba juu yake wakat alipoanza siasa.
“Karibu tena Uraini brother!{nakumbuka uliwahi kuimba juu yangu wakati huo nilipoanza siasa},” ameandika Nape kupitia ukurasa wake Twitter.
Sugu na katibu wa Chadema kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela February 26, 2018 kwa kutoa lugha ya fedhea dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desember 30, 2017 katika uwanja wa shule ya msingi Mwenge, Mbeya
Post A Comment: