Mahakama ya Hakimu Mkazi, Iringa, imepokea vielelezo vya kimtandao vilivyoletwa na upande wa mashtaka dhidi ya Mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) Abdul Nondo.
Akizungumza Mahakamani hapo, leo Mei 10, Hakimu Mkazi, wa mahakama hiyo, John Mpitanjia amesema amepokea vielelezo hivyo baada ya kupitia sheria mbalimbali za mitandao ya kijamii.
Mpitanjia amesema, mahakama inawajibu wa kupokea kila kielelezo kinachokuja mbele yake.
Baada ya uamuzi huo upande wa utetezi chini Wakili Chance Luoga uliridhia maamuzi hayo na kuomba kesi hiyo iendelee tena Mei 14
Nondo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu,(TSN) anakabiliwa anakabiliwa na mashtaka mawili shtaka la kwanza ni kusambaza taarifa za uongo akiwa jijini Dar es Salaam kuwa ametekwa na kosa la pili ni kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.
Post A Comment: