Jeshi la Magereza limesema mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ametoka kwa msamaha wa Rais John Magufuli alioutoa kwa wafungwa katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Aprili 26, 2018.
Ofisa habari wa jeshi hilo, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje amesema katika maadhimisho hayo, Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 3,319, kati yao wafungwa 585 waliachiliwa huru Aprili 26, 2018.
“Wafungwa 2,734 walibakia gerezani akiwemo Sugu kumalizia sehemu ya kifungo kilichobakia baada ya kupewa msamaha huo na Rais Magufuli,” amesema.
Post A Comment: