Na Ramadhan Ali - Maelezo
Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA) imegundua udanganyifu uliokuwa ukifanywa na mfanyabiashara Ujudi Abass wa kubadilisha utambulisho (brand) wa mafuta ya kula ya TURKEY na kuweka utambulisho wa  OKI kinyume na sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ZFDA Dkt. Khamis Ali amesema udanganyifu huo uliokuwa ukifanywa ndani ya Tawi la CCM Makadsara ulibainika baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Alisema utambulisho wa OKI uliokuwa ukitumiwa  kinyume na sheria na mfanyabiashara huyo ulikuwa wa kughushi na lengo lake kubwa ni kutafuta soka na bei ya juu katika masoko ya Dar e salaam ambako  hivi sasa kunaupungufu wa mafuta hayo.

Dkt. Khamis alisema kuwa mafuta hayo, zaidi ya galoni 747, yanatoka nchini Indonesia na yalizalishwa mwezi Mei mwaka 2017 na muda  wa mwisho wa matimizi ni mwezi Mei mwaka 2019 hivyo yapo salama kwa ajili ya matumizi na kosa la mfanyabiashara huyo ni kubadilisha utambulisho halali wa TURKEY na kuweka utambulisho wa Kampuni nyengine

Alisema mfanyabiashara Ujudi Abss hivi sasa anashikiliwa na vyombo vya ulinzi na  anatarajiwa kufikishwa katika vyombo vya sheria wakati wowote kujibu tuhuma za udanganyifu.

Mwakilishi wa Kampuni ya Sahara ambao ni wakala wa OKI ameeleza kusikitishwa na kitendo cha  udanganyifu   uliofanywa na mfanyabiashara huyo kutumia stika za kampuni hiyo kwa lengo la kutafuta kipato kwa vile mafuta ya OKI ni maarufu na yanasoko.

Alisema kitendo cha kutumia stika ya kampuni kwa biashara nyengine kwa njia  udanganyifu kinaweza kushusha hadhi ya biashara  halisi na  kupoteza imani kwa watumiaji. 
Share To:

msumbanews

Post A Comment: