Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa kuna Kampuni iko Mwanza iliingia Mkataba na King Majuto na Mkataba huo ulikuwa ni wakumlipa Milioni 24 wakatoa check, check hiyo ikawa haina Pesa, Hivyo serikali imewachukulia hatua wahusika.
“Naomba niwaeleze wananchi Nimeunda jopo la wanasheria na tumeshaanza kikao cha kwanza sasa hivi kazi yetu kubwa kwasababu tumeshaanza na suala la Mzee Majuto ni kuangalia kazi zote alizokwisha zifanya na tunawaandikia barua wote waliohusika watupe mikataba wanayoijua wao tutakaa nao tuanza kuchambua mkataba mmoja baada mwingine na tutawataarifu itakavyo fuatia,” amesema Dkt. Mwakyembe
“Kuna kampuni moja ya Mwanza waliingia Mkataba na King Majuto na Mkataba huo ulikuwa ni wakumlipa Milioni 24 wakatoa check, check hiyo ikawa haina Pesa tunashukuru uongozi wa Mwanza kwa kushirikiana nao wahusika wako ndani na tutaendelea kuchukua hatua kali kwa watu ambao wanadhani wanaweza kutumia jasho la wenzao kujinufaisha wenyewe,” alisisitiza.
Post A Comment: