Majogoo wa Anfield wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya AS Roma ya Italy.
Liverpool imetinga hatua hiyo baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-2 ugenini, lakini inasonga mbele kufuatia ushindi wa 5-2 katika mechi ya mkondo wa kwanza ikiwa nyumbani.
Liverpool imejipatia mabao yake kupitia kwa Sadio Mane pamoja na Wijnaldum, hivyo imekuwa tiketi ya kukutana na Real Madrid kwenye fainali huko Kiev.
Madrid ilikuwa ya kwanza kuingia hatua ya fainali kufuatia kuiondosha Bayern Munich kwa idaidi ya mabao 4-3.
Post A Comment: