Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeadhimia kuligawa Jimbo la Mbagala liliopo Jijini Dar es Salaam baada ya kuwepo kwa idadi kubwa ya wakazi wanaoishi jimboni humo na kusababisha uhaba wa upatikaji wa huduma za muhimu kutoka kwa Mbunge wao.
Kauli hiyo imetolewa leo Mei 11, 2018 na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph Kakunda Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 27 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la nyongeza la Mbunge Mariam Kisangi aliyetaka kujua serikali inamkakati gani wa kuligawanya Jimbo la Mbagala ili liweze kufikika kiurahisi na hata Mbunge wao aweze kutoa kwa wananchi kwa wakati.
"Ni kweli Jimbo la Mbagala kwa idadi ya watu ni miongoni mwa majimbo yenye watu wengi zaidi hasa ya Dar es Salaam, lakini hivi karibuni tumeyagawa majimbo ya jiji hilo.
"Kwa hiyo mimi nilikuwa nashauri kwa vigezo vile ambavyo nimevizungumza katika majibu ya msingi, ninaomba sasa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wakae na waweze kupendekeza na mwishowe wapeleke mapendekezo yao moja kwa moja katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)", amesema Kakunda.
Kwa mujibu wa Mbunge Mariam Kisangi amesema Jimbo la Mbagala mpaka hivi sasa lina jumla ya wananchi Milioni moja na laki moja jambo ambalo linapelekea utoaji wa huduma kuwa mgumu pamoja na kuharibika kwa miundombinu mara kwa mara kutokana na wingi wa watu waliopo jimboni humo.
Post A Comment: