Maeneo ya katikati ya Jiji la Mwanza leo Mei 11, 2018 yatakosa umeme kwa saa nane baada ya transfoma na nyaya za umeme kuanguka eneo la Kauma na kuziba barabara ya stesheni.

Kwa mujibu wa taarifa ya  Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) zinaeleza kuwa nishati hiyo itarejea kuanzia saa 11 jioni.

Ofisa uhusiano wa Tanesco jijini Mwanza, Flaviana Moshi amesema nguzo hizo zimedondoka saa 2 asubuhi na kuathiri upatikanaji wa umeme kwa maeneo mengi ya jiji hilo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: