Mbunge wa Vunjo James Mbatia ambaye ni mdau mkubwa wa elimu amesema kwamba  umefika wakati wa kukubali kuwa hali ya elimu ya Tanzania ni janga hivyo mjadala ufanyike kama walivyoshauri marais wastaafu.

Mbunge huyo ameyasema hayo bungeni wakati  akichangia hoja katika bajeti ya wizara ya elimu, iliyowasilishwa Bungeni na waziri mwenye dhamana, Pro. Joyce Ndalichako.

"Mzee Mkapa amesema kwamba elimu yetu tunahitaji mjadala wa kitaifa. Mzee Kikwete naye ametamka . Sasa nani mwingine atamke zaidi mpaka tuhakikishe kwamba tunaangamia elimu yetu?" Mbatia.

Ameongeza "Mh. Mwenyekiti niseme 'The way Foward' tukubali elimu yetu tupo kwenye janga ni maafa na ukiwa na maafa naomba tusiwe na tofauti za kiitikadi huku ndani. Tusimame  sote kwa pamoja na Mh. Waziri yote tunayoyasema naomba uyachukulie very positive kwa ajili ya kujenga Taifa letu, Wizara yetu pamoja na kujenga watoto wetu na kizazi chetu".

Hata hivyo Wabunge wanatarajiwa kujadili na kuipitisha bajeti ya wizara ya elimu sayansi na teknolojia ya zaidi ya shilingi trilioni 1.4 kwa mwaka wa fedha 2018/2019
Share To:

msumbanews

Post A Comment: