Mnamo May 6, 2017 Tanzania ilizizima kwa taarifa za ajali iliyohusisha basi la wanafunzi wa shule ya Lucky Vincent ambayo iliua wanafunzi 29, dereva na walimu wawili huko katika mlima Rhotia wilayani Karatu Mkoani Arusha.

Jana May 6 ilikuwa ni kumbukumbu ya mwaka mmoja tangu kutokea kwa ajali hiyo iliyobakiza wanafunzi watatu tu waliokuwa kwenye basi hilo.

Katika kumbukumbu hiyo shule ya Lucky Vincent imefanya ibada maalumu ya kuwakumbuka wanafunzi pamoja na waalimu waliofariki kwenye ajali hiyo.

Umejengwa mnara katika eneo la mlima huo wa Rhotia ambapo ndipo gari hilo lilipopata ajali. Mnara huo una majina ya watoto wote waliofariki kwenye ajali hiyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: