Muongozaji wa video za muziki nchini Tanzania, Hancana amefunguka na kumkataa msanii wa BongoFleva Darassa kwamba hajawahi kuwa msemaji wake wala kumsimamia kazi zake za sanaa hapo awali bali yeye alikuwa ni muongozaji tu katika kazi ambazo aliwahi kufanya kwake.
Hancana ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz kinachorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV baada ya watu wengi kudai muongozaji huyo anahusika kwa namna moja ama nyingine katika usimamizi wa kazi za Darassa huku wengine wakienda mbali zaidi kuwa pia anafahamu chanzo cha kupotea msanii huyo katika 'game' ya muziki.
"Sihusiki kuongelea jambo lolote linalo muhusu Darassa kwasababu yeye ni 'brand' na mimi sio msemaji wa 'brand' ya Darassa bali mimi ni rafiki tu. So kama yeye ni 'brand' inabidi ajitokeze mwenyewe na kujizungumzia yeye kama yeye. Haitakuwa sahihi Hancana kuzungumzia brand ya mtu mwingine", amesema Hancana.
Mbali na hilo, Hancana amempongeza Darassa kwa kuweza kuhimili miki ya vitu vyote ambavyo watu walikuwa wanampakazia hasa kuhusu kujihusisha na dawa za kulevya.
"Nadhani hizi skendo huja kumpanikisha mtu ili wapate kumsikia anasemaje, 'sometimes' hivyo vitu vipo. Ninachomshukuru Darassa au kumpongeza ni amekuwa 'very strong' amesimama kwenye mipango yake anayoiamini 'no matter what', watu wanampanikisha kwamba anatumia dawa za kulevya mara amepotezwa kwenye muziki", amesisitiza Hancana.
Post A Comment: