Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka sababu ya kutompa mkono Alikiba walipokutana katika msiba wa Agness Gerald ‘Masogange’.

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na ngoma ‘Kwa Ngwaru’ ameiambia The Playlist ya Times FM kuwa mambo yote yanayozungumzwa si ya kweli, bali walisalimiana ila si kwa kushikana mikono.

“Unajua asilimia kubwa ya watu wanaozungumza hawakuwa pale, unajua unapomzungumzia Alikiba ni mtu ambaye amefanya muziki wetu upate heshima kwa namna moja au nyingine, kama msanii namheshimu siwezi nikakutana na mtu halafu nisimsalimie, sio kweli,” amesema na kuongeza:

“Kilichofanyika ni kwamba Diamond kamsalimia kwa mkono, wamesamiliana kwa mkono. Mimi nimekuja nimezunguka nikaona kwa kuwa Diamond kamsalimia kwa mkono, kamgeuzia kiganja, mimi nikamsalimia kwa sauti tu, tukakaa pale tukaendelea.” .
Share To:

msumbanews

Post A Comment: