Halmashauri ya wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza imepokea zaidi ya vitabu elfu sitini kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu na hivyo kusaidia kufikiwa lengo la kila mwanafunzi kutumia kitabu kimoja.
Zoezi la upokeaji na ugawaji wa vitabu hivyo, limefanyika hii leo katika shule ya msingi Misungwi likiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Mhe.Juma Sweda ambaye amewataka waalimu kuhakikisha vitabu hivyo vinatumika kama ilivyokusudiwa huku pia akiwataka wazazi kuhakikisha watoto wao wanahudhuria shule kila siku badala ya kwenda kuchunga mifugo.
Afisa elimu msingi wilayani Misungwi, Mwl.Ephraim Majinge amesema mwaka huu wilaya hiyo imepokea jumla ya vitabu vya kiada 63,354 kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu vilivyotolewa na Rais Dkt.John Magufuli kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na hivyo kusaidia uwiano wa mwanafunzi mmoja, kitabu kimoja.
Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Juma Sweda akizindua zoezi la upokeaji na ugawaji vitabu katika shule zote za msingi 139 wilayani humo.Mkuu wa wilaya ya Misungwi Juma Sweda (katikati), Afisa Elimu Msingi wilayani Misungwi Mwl.Ephraim Majinge (kushoto) pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii Halmashauri ya Misungwi Ngagizi Zozozo (kulia) wakionyesha vitabu hivyo.Viongozi mbalimbali wakionyesha vitabu hivyo.Mkuu wa wilaya ya Misungwi, Mhe.Juma Sweda akizungumza kwenye zoezi la upokeaji na ugawaji vitabu wilayani humo.Afisa Elimu Msingi wilayani Misungwi, Mwl.Ephraim Majinge akitoa taarifa kuhusiana na vitabu hivyo.
Post A Comment: