Chama cha soka nchini Uingereza FA kimeipiga faini ya pauni 20,000 klabu ya Arsenal kufuatia wachezaji wake kumgasi mwamuzi baada ya kuipatia penati timu ya Leicester.

Arsenal imelimwa faini hiyo ya pauni 20,000 kufuatia baadhi ya wachezaji wake kuonyesha kitendo cha utovu wa nidhamu kwa kumgasi mwamuzi, Graham Scott wakionyesha kutoridhishwa na maamuzi aliyofanya ya kuwapatia Leicester penati dakika ya 75, kwenye mchezo wao uliyopigwa Mei 9.

FA ameipatia adhabu The Gunners mapema mwezi huu baada ya idadi kubwa ya wachezaji wake kumzonga mwamuzi huyo wakati akiwazawadia penati Mbweha hao wa Uingereza ‘the Foxes’.

Kwenye mchezo huo Jamie Vardy  alitupia bao huku Leicester wakiwa nyumbani King Power Stadium wakifanikiwa kuchomoza na ushindi wa mabao 3 – 1 dhidi ya Arsenal.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: