Msanii Ebitoke amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake anamchukia sana mwanaharakati wa mitandao Mange Kimambi na kusema kuwa alimkwaza sana kuingilia maisha yake na kusababisha mashabiki wake washindwe kumuelewa kuhusu tuhuma za yeye kuiba mume wa Mama Ashura.

Ebitoke amesema hayo leo Mei 9, 2018 katika kipindi cha Kikaangoni  kinachorushwa na  EATV na kusema kuwa mwanadada huyo aliingia katika anga zake na kumchefua kabisa jambo ambalio liliongeza kumchukia.

"Kwanza yule dada Mange Kimambi mimi simpendi, sijawahi kabisaa kumkubali, sipendi mambo yake na sipendi vimtu vinavyoongea sana, yule dada aliingilia maisha yangu na kunichafulia mpaka kwa mashabiki zangu saizi wengine wanashindwa kunielewa. Mange Kimambi mimi siyo size yangu kabisaa kwanza yeye mtu mzima sasa nilishangaa kwanini yeye anaingilia maisha yangu" alisema Ebitoke.

Mbali na hilo Ebitoke aliweza kutoa ushauri wake kwa mwanaharakati huyo wa mitandaoni Mange Kimambi na kusema kuwa asifanye mambo ya kufuatilia maisha ya watu bali afanye mambo yake mengine.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: