CHUO
cha Uhasibu Arusha(AII)kinatarajia kuanzisha programu mpya nne za
Uzamili kwa fani ambazo zitawawezesha wahitimu kukubalika kwa urahisi
katika soko la ajira za moja kwa moja nchini.
Hayo
yamesemwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo Uhasibu Arusha Dk. Samwel
Welema wakati anazungumza na wadau kutoka katika mashirika na kampuni
mbalimbali za binafsi na Serikali katika warsha iliyofanyika kwenye Chuo
hicho Kitivo cha Dar es Salaam.
Amefafanua
kuanzishwa kwa program hizo kitakiwezesha chuo hicho kujihakikishia
kwamba kile kinachofundishwa kitaenda kutumika na kinauhitaji mkubwa
kwenye soko la ajira.
Dk.Welema
amezitaja programu hizo ni Master of Science and
Investment(MScFI),Master in Business Administration(MBA), Master in
Business Administration in Information Technology Management(MBA-ITM) na
Master of Business Administration in Procurement and Supplies
Management(MBA- PSM)
Kwa
upande wa Mkuu wa Idara ya Masomo ya Uzamili chuoni hapo, Grace Temba
amesema, michango na maoni mbalimbali waliyoipata kutoka kwa wadau
wakitaka kuanzishwa kwa program hizo mpya na ndio sababu ya chuo hicho
kuona haja ya kuanzisha program hizo.
"Kwa
kipindi cha miaka mitatu...minne, tumeweza kuongeza kusomesha walimu
wetu hadi kufikia 16 ambao wanadigrii na wapo tayari kutoa elimu kwa
hatua ya Uzamili" amesema Temba.
Amesema,
wamepata maoni kutoka kwa wawakilishi wa mashirika na kampuni mbali
mbali na lengo kuu ni kuhakikisha kile ambacho kinaenda kutumika
kinamahitaji kwenye soko la ajira.
Ameongeza,
wahitimu wengi wanamaliza wakiwa wanajua nadharia tu, lakini sasa chuo
kitakuwa kinatoa mafunzo kwa vitendo ambapo wahitimu watakuwa na uwezo
mkubwa ukiwemo kuandaa ripoti, kusaidia kampuni na kuchanganua masuala
mbalimbali kwa manufaa ya kampuni.
Kaimu
Mkuu wa chuo cha Uhasibu cha Arusha, (AII), Dk. Samwel Welema
akizungumza na wadau kutoka mashirika na makampuni mbali mbali nchini,
juu ya azma ya chuo hicho kuanzisha programu nne za uzamili, katika
warsha iliyofanyika katika chuo hicho kitivo cha Dar es Salaam.
Mhadhiri
wa chuo cha Uhasibu Arusha Kitivo cha Dar es Salaam, Allan Msola
akiwaelezea wadau kutoka mashirika na makampuni mbali mbali nchini juu
ya programu nne za uzamili zinazotarajiwa kuanzishwa na chuo hicho hivi
karibuni hapa nchini, katika warsha iliyofanyika katika chuo hicho
kitivo cha Dar es Salaam.
Wadau na washiriki kutoka kwenye makampuni na mashirika mbali mbali wakifuatilia kwa making warsha iliyotolewa na chuo cha Uhasibu Arusha (AII) juu ya namna program mpya za uzamili zinazotarajiwa kuanzishwa na chuo hicho zitakavyowanufaisha wahitimu na makampuni watakayoenda kufanyia kazi.
Wadau na washiriki kutoka kwenye makampuni na mashirika mbali mbali wakifuatilia kwa making warsha iliyotolewa na chuo cha Uhasibu Arusha (AII) juu ya namna program mpya za uzamili zinazotarajiwa kuanzishwa na chuo hicho zitakavyowanufaisha wahitimu na makampuni watakayoenda kufanyia kazi.
Mkuu
wa Idara ya masomo ya Uzamili wa chuo cha Uhasibu Arusha(AII), Grace
Temba,akifafanua juu namna Program mpya zinazotarajiwa kuanzishwa na
chuo hicho zitakavyofanya kazi na kuwawezesha wahitimu kukubalika moja
kwa moja kwenye soko la ajira ndani na nje ya nchi
Post A Comment: