MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mtwara leo Ijumaa Mei 4, 2018 imetoa zuio la muda (Temporary Injuction) dhidi ya matumizi ya kanuni mpya za Maudhui ya Kimtandao (Online Content Regulations) ambazo matumizi yake yamekwishaanza ambapo kesho Mei 5, 2018 ndiyo siku ya mwisho kwa blogers na wamiliki wa majukwaa ya mitandaoni (Online Forums) kusajili huduma hizo kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Maombi ya zuio hilo yaliyowalishwa mahakamani na waombaji sita wakiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (Legal and Human Rights Cente -LHRC), THRDC, MCT, TAMWA, Jamii Media na TEF ambapo katika kesi ya msingi ya mapatio ya kanuni hizo (Judicial review) washitakiwa ni Waziri wa Habari, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (Tanzania Communication Authority -TCRA) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)
.
Aidha, katika maombi ya msingi, waombaji wameiomba Mahakama kufanya mapitio ya kanuni hizo kwa vigezo vifuatavyo;
i) Waziri wa Habari ametumia nguvu ya kisheria nje ya mamlaka yake (Ultra vires).
ii) Kanuni hizo zinakiuka kanuni za usawa (Natural justice).

iii) Kanuni hizo zinapingana na Uhuru wa kujieleza (Freedom of Expression) Haki ya kusikilizwa(Rights to be heard) na haki ya usiri( Right to Privacy)
Katika kesi ya msingi, shauri hilo limepangwa kusikilizwa tarehe Mei 10, 2018.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: