Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam na Meneja wa mwanamuziki Naseeb Abadul ‘Diamond’, Hamis Taletale ‘Babu Tale’, leo amefikishwa katika Mahakama Kuu jijini Dar ambako baada ya hakimu aliyetoa amri ya kumkamata kutokuwepo kesi imeharishwa na Babu Tale atarudishwa mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.

Kipindi cha nyuma mahakama hiyo ilimwamuru Babu Tale alipe Sh. milioni 250 Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi hicho baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18, mwaka juzi, katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde aliyewalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: