Kikosi cha Azam FC kinashuka dimbani usiku wa saa moja leo kucheza dhidi ya Majimaji FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara.

Azam ambayo imeungana na Yanga kugombania nafasi ya pili hivi sasa, itakuwa inawakaribisha Majimaji ambao wanapambana kuepuka kushuka daraja.

Ofisa wa Habari wa Azam FC, Jaffer Idd Maganga, amesema kuwa kuifikia Simba hivi sasa imeshakuwa ndoto hivyo itawabidi kuchuana na Yanga ili kukalia kiti cha nafasi ya pili.

Maganga amesema tayari Simba ameshakuwa bingwa na ni ndoto kumfikia hivyo ni vema wakapamba washike nafasi ya pili.

Azam ambao wana michezo miwili mbele ya Yanga wamejikusanyia alama 49 wakiwa nafasi ya pili huku Yanga wakiwa na pointi 48 kwenye nafasi ya tatu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: