Kikosi cha Azam Fc kimekubali kichapo cha bao 2-1 kutoka kwa wapiga debe wa Stand United kutoka Shinyanga.

Mabao ya Stand yamefungwa na Sabilo pamoja na Ally huku bao pekee la Azam likitiwa nyavuni na Shaaban Idd.

Matokeo mengine ni Kagera Sugar iliyokuwa nyumbani Kaitaba Stadium imelazimishwa suluhu ya kutofungana na Mbeya City.

Wakati huo Majimaji nayo ilikuwa inawaalika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Majimaji na mechi hiyo ikamalizika kwa matokeo ya 0-0.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: