Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba maarufu kama King Kiba, ameeleza sababu inayomfanya kutoa wimbo baada ya muda mrefu.

Kiba amesema kuwa anafanya hivyo kutokana na kutokuua soko la muziki wake kufanya vizuri, hivyo haoni sababu ya kutoa kila wakati baada ya muda mfupi.

Akizungumza kupitia Power Breakfast ya Clouds FM, Kiba amesema ili kutokuua soko la muziki, haoni haja ya kufululiza nyimbo kama wimbo wake unafanya vizuri kwa muda mrefu.

"Sababu kuwa inayonifanya sitoi wimbo baada ya muda mfupi ni kutokuua soko la muziki wangu, kama wimbo niliotoa unafanya vizuri na unaingiza faida hakuna haja ya kuwa na uharaka wa kutoa tena mwingine" amesema Kiba.

Mara ya mwisho Kiba kutoa wimbo ambao unajulikana kwa jina la Seduce Me, ilikuwa ni Agosti 25 2017.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: