Na Ferdinand Shayo,Kilimanjaro.
Mkoa wa Kilimanjaro umekubwa na changamoto ya vibao vya alama za barabarani kung`olewa na baadhi ya watu wasiofahamika jambo ambalo linaisababishia hasara Tanroad na serikali kwa ujumla.

Meneja wa Tanroad  Ntije Nkolante amesema amekiri kutokea kwa matukio hayo ya mara kwa mara ya alama za barabarani kuondolewa jambo ambalo linaweza kuleta matumizi mabaya ya barabara  na hata kusababisha ajali.

Meneja huyo amewataka Wananchi kutoa taarifa kwa wanaohusika na uharibifu huo ili waweze kuchukuliwa  hatua kali za kisheria .

Hata hivyo amesema kuwa bado hasara inayosababishwa na uharibifu haijajulikana hivyo watafanya tathimini na kutoa taarifa rasmi.

Baadhi ya Wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro Damas Michael na Happy Micky wamesema kuwa kitendo hicho ni kuhujumu maendeleo na juhudi za wananchi wanaolipa kodi ili waweze kupata barabara bora
Share To:

msumbanews

Post A Comment: