Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya amewataka madereva bodaboda kuwapiga picha abiria wao kabla hawajaanza safari, kwa ajili ya usalama wao.

Lucas Mkonda ametoa rai hiyo kufuatia tukio la kuokotwa kwa mwili wa dereva boda boda Ally Rashidi Kitima, mkazi wa Magomeni Chipuputa mkoani Mtwara, katika eneo la Shule ya Sekondari ya Mtwara Islamic siku chache baada ya kupotea.

Kwa mujibu wa Kamanda Mkondya amesema kwamba kufanya hivyo kutawasaidia kupata taarifa za mtu ambaye alimpakia mwisho iwapo atakutwa na tukio lolote na kuweza kusaidia kufanya uchunguzi, na kwamba uchunguzi juu ya tukio la kifo cha dereva boda boda Ally Rashidi bado unaendelea.

Naye jirani wa marehemu Sele Kumbo amesema kwamba siku chache zilizopita marehemu alipata abiria na kumpeleka maeneo ya shule ya Mtwara Islamic na hakurudi tena, mpaka mwili wake ulipoonekana siku ya tarehe 18 May, 2018.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: