Serikali kupitia Waziri wake wa Nishati Dk. Medard Kalemani amesema kuanzia leo gesi asilia toka mikoa ya kusini itaanza kusambazwa majumbani katika baadhi ya maeneo jijini Dar es salaam.
Gharama ya kuunganisha gesi kwa wateja watakaopitiwa na bomba la gesi itaanzia Shilingi laki mbili (200,000) mpaka Milioni moja (1000,000) pesa ya kitanzania, gharama hizo zitatofautiana kulingana na umbali uliopo kutokea bomba lilipopita.
Baadhi ya maeneo yatakayofikiwa na gesi hiyo yametajwa kuwa ni Ubungo, Ubungo Maziwa, Chuo Kikuu, Kijitonyama, Mwenge, Gongolamboto, Mikocheni na Shekilango gharama hizo zikiwa ni punguzo la asilimia 40 kulinganisha na gesi ya mitungi inavyotumiwa hivi sasa.
Kalemani ametoa kauli hiyo pindi akijibu hoja ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alipouuliza kuhusu mkakati wa Wizara hiyo
Post A Comment: