Kikosi cha Zesco United jana kimeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu nchini Zambia 'Zambia Super League' kwa kuilaza Power Dynamos kwa mabao 2-1 ikiwa Uwanja wake wa nyumbani, Levy Mwanawasa.

Mabao ya Zesco yalifungwa na Lazarus Kambole aliyeingia kambani mara mbili katika dakika za 49 na 65 huku bao la Power Dynamos likitiwa kimiani na Kelvin Mubanga kwenye dakika ya 6 ya mchezo.

Ushindi huo umekuwa wa pili mfululizo baada ya Kocha George Lwandamina kurejea klabuni hapo ambapo mechi iliyopita dhidi ya Lusaka Dynamos, Zesco iliibuka na ushindi wa bao 1-0 ikiwa ugenini.

Msimamo wa ligi unaonesha Zesco imekata nafasi ya pili ikiwa imecheza michezo mitano nyuma ya Green Buffaloes iliyo mbele kwa mechi moja, ambapo Zesco imejikusanyia alama 13 huku Buffaloes wakiwa na 16
Share To:

msumbanews

Post A Comment: